Burudani

Linex akanusha kuwa na uhusiano na Agnes Masogange ‘I’m single na sina haraka ya kuwa na mpenzi’

So Linex Sunday Mjeda sasa ana mpenzi mpya mtoto mzuri wa hapa town aitwaye Agnes Masogange?? NO! hilo ndiyo jibu la Linex hivyo ‘Kuweni na Subira’, sababu kwa sasa yuko single.

Agnes Masogange akiwa na Linex

Mwana Lekadutigite Linex a.k.a The V.O.A amekanusha habari zilizoenezwa jana kuwa ana uhusiano mpya wa kimapenzi na Video Vixen mwenye ‘assets’ zinazowasumbua wanaume wengi Agnes Gerald maarufu kama Agnes Msambinungwa Masogange.

linex n aggy-2

Habari hizo zilianza kuenea baada ya Linex na Agnes kupost picha walizopiga pamoja weekend iliyopita katika maeneo mawili tofauti, ya kwanza ikiwa katika mechi ya mpira wa kikapu kati ya timu za madirector wa video Adam Juma na Karabani, na nyingine wakiwa ufukweni wakipunga upepo.

linex n aggy-3
Linex ameweka wazi status yake ya uhusiano kwa sasa kama njia ya kukanusha uvumi huo,

“Boss Ngasa Official Website: HATIMAYE AGNESS MASOGANGE NA LINEX NDANI YA MAPENZI MAZITO…..!! TAZAMA PICHA WAKILA BATA WAPENZI HAWA…!! – http://www.bossngasa.com/2014/02/hatimaye-agness-masogange-na-linex.html?m=1 ni kweli watu wa blog mnapush sana kazi zetu but nimesikitishwa na habari hii iliyoandikwa na blog kadhaa mtasababisha tutashindwa ata kukaa na Dada zetu au marafiki zetu Uliza b4 Hujaandika ujinga am single na sina haraka ya kua na mpenzi.” Aliandika Linex kwenye akaunti yake ya facebook.

Katika moja ya picha za ufukweni Agnes alizopost pia aliandika ‘With my frnd mjeda nishida tupu Leo na Cheus wangu @linexsundaymjeda #Beach life’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents