Listi ya klabu 100 tajiri Afrika yaanikwa, timu mbili zatoka Afrika Mashariki
Kampuni ya ‘Finances of Football’ imetangaza listi ya klabu 100 tajiri barani Afrika huku kila moja ikipangwa kutokana na kipato chake pamoja na matumizi yake.
Makao makuu ya klabu ya Simba yaliyopo mitaa ya Karia Koo
Kwamujibu wa Finances of Football, Afrika Mashariki zimetoa klabu mbili pekee ambazo ni Simba SC ya Tanzania ikiwa nafasi ya 60, huku ikikadiriwa kuwa dola za Kimaarekani 2,230,050 na Gor Mahia kutoka Kenya ikiwa ya 78 ikiwa na kiasi cha dola 1844585.
Kwenye listi hiyo timu ya Al Ahly inaongoza kwa kushika nafasi ya kwanza ikikadiriwa kuwa dola za Kimarekani milioni 28, ikifatiwa na Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini ikiwa na dola milioni 23 nafasi ya tatu ikishikiliwa na Pyramids wakati ya nne ikienda kwa Club African na ya tano ikishikiliwa na Zamalek yenye dola za Kimarekani milioni 18.and Orlando Pirates.
Hakuna klabu yoyote kutoka Rwanda ,Uganda wala Malawi zilizoingia kwenye listi hiyo wakati TP Mazembe ikiwa ni klabu pekee kutoka Kongo iliyoingia nafasi ya 10.
Kwa mujibu wa Finances of Football listi ya klabu hizo 100 zimepangwa kulingana na akaunti za klabu pamoja na bajeti zao za mwaka kutoka katika vyonza vya kuaminika.
Latest #African Club #RichList. Based on club accounts & also annual budgets from reliable sources. As ever South African #PSL and the North African clubs dominate. NOTE #PyramidsFC figure is based on 400m EGP sponsor, with the politics at this club currently this may be invalid. pic.twitter.com/yUKxmkLTOC
— Finances of Football (@financesoffooty) November 14, 2018
Selected others .. pic.twitter.com/euLt748xLd
— Finances of Football (@financesoffooty) November 14, 2018
Kikosi cha wachezaji wa Simba