Habari

Lupita Nyong’o afikisha followers milioni 1 Intagram

Mwigizaji wa Kenya Lupita Nyong’o ameweka rekodi nyingine kwa kufikisha followers milioni 1 katika mtandao wa Instagram ambao mpaka leo tayari ana 1,007,570.

480854031CC00168_2014_MTV_M

Kwa mujibu wa Nairobi Wire, Lupita ndio amekuwa Mkenya wa kwanza kufikisha followers wengi Instagram, huku upande wa Facebook mchekeshaji wa Kenya Daniel Churchill ndiye Mkenya wa kwanza aliyefikisha likes Millioni moja wiki iliyopita.

Mastaa wengine wa Kenya ambao wameachwa mbali na Lupita kwa kuwa na followers wachache Instagram ni pamoja na Prezzo mwenye 28,000+ Victoria Kimani ambaye ana 17,000+ na video vixen Vera Sidika ambaye ana 15,000+.

Kwa upande wa Tanzania Diamond Platnumz na Wema Sepetu ndio mastaa wenye followers wengi zaidi, Diamond akiwa na 106,000+ na mpenzi wake Wema akiwa na 95,000+.

Tazama jinsi Lupita alivyoshangilia baada ya kufikisha followers M1

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents