Burudani

Madee aeleza siri ya wimbo wake mpya ‘Hela’ kufanya vizuri

Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Madee Ali amefunguka kwa kudai kuwa wimbo wake mpya ‘Hela’ unafanya vizuri kutokana na jinsi alivyobadika kwenye kuiamba.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Madee amedai aligundua mashabiki wake wanataka nini ndiyo maana akabadilika na kufanya kitu tofauti.

“Mimi nafanya muziki kama biashara, nikiona kitu hiki nimefanya kwa muda mrefu najua hapa natakiwa kubadilika kwa sababu hata mashabiki nao wanataka vitu tofauti, kwa hiyo baada ya kuona kuna ngoma kadhaa nimefanya kwa mtindo fulani sasa hivi sitaki nije vile vile tena ndio maana nimebadilikana na mambo yamekuwa mazuri,” alisema Madee.

Aliongeza, “Kwa hiyo binafsi niliona mashabiki wangu kuna kitu fulani wanakitaka, ndio maana nimebadilika kidogo na kweli ngoma imefanya vizuri sana,”

Pia muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kuendelea kukaa mkao wa kula kwajili ya kazi mpya ambazo zitatoka hivi karibuni baada ya Dogo Janja kuachia project mpya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents