Habari

Maisha baada ya BBA: Mpenzi wa Selly ataka Nando akamatwe na afungwe kwa kosa la kutishia kuua!

Ilianzia ndani ya jumba la Biggie na sasa inaendelea nje ya mjengo wa Big Brother, ni kati ya aliyekuwa mshiriki wa Tanzania katika ‘The Chase’ Amy Nando dhidi ya Waghana.

Bull-Dog
Bull Dog

Tukirudi nyuma kidogo katika historia ya The Chase kuangalia uhusiano kati ya Nando na waghana, kwanza mpenzi wa Nando mjengoni Selly alikuwa mshiriki wa Ghana, pili Nando ametolewa mchezoni baada ya ugomvi baina yake na Elikem ambaye pia ni mshiriki wa Ghana, na sasa mpenzi wa Selly (aliyeibiwa mpenzi na Nando) naye anamekuja kwenye picha hii.

Baada ya Selly na Nando kutoka katika ‘The Chase’ inaonekana sasa mambo yanaingia katika awamu nyingine baada ya boyfriend wa mshiriki wa Ghana Selly kusema Nando anastahili kushitakiwa kwa kumtishia kumuua Elikem kitendo kilichopelekea Nando kupata adhabu ya kuondolewa mchezoni kwa kukiuka masharti ya mchezo.

Lawrence Nana Asiama Hanson a.k.a Bull Dog ambaye ni boyfriend wa Selly wa Ghana ametoa maoni yake kwa polisi wa Afrika Kusini kumfungulia mashitaka Nando sababu anaamini kuwa kumtishia mtu kumuua ni sawa na kutenda kosa la mauaji, na kuongeza kuwa kama Nando alitamka nia yake ya kumuondoa uhai Elikem akiwa mjengoni kuna uwezekano akaamua kuendelea na mpango huo hata baada ya kutoka mjengoni,

“For me, I think disqualifying Nando from the competition is not enough. The Police there should arrest and jail him because threatening to kill someone is equally an offence as murder. Once he has said that he feels like stabbing Elikem, it means that outside the Big Brother House, Nando might go ahead and finish what he said he will do,” Alisema Bull Dog alipohojiwa na NEWS-ONE

Alichokisema Bull Dog kinatokana na kauli ya Nando aliyoitoa wiki iliyopita baada ya kutoelewana na Elikem “I swear. I felt like stabbing that n*gga. These are the n*ggas that deserve to die.”

Mtandao wa Highlife Today umeandika baadhi ya maoni ya mashabiki kutoka Ghana ambao mmoja wao amedai sio jambo la kawaida kwa mtu (Nando) kutishia kuchoma visu watu kila wanapotofautiana.
“It was not the first time Nando has done such a thing. The first time, he had the intention of stabbing Sulu. Now he opens his big mouth and threatens to stab and kill Elikem. It seems he has a mental problem.” Alitweet mmoja wa mashabiki hao.

Bull Dog aliongeza kuwa hata kama Nando ana matatizo ya kisaikolojia lakini hakupaswa kutishia uhai wa mtu sababu ni kinyume cha sheria.

Nando
Nando

Nando ambaye tayari amerejea Tanzania alifanyiwa mahojiano na Clouds FM Jumatano (July 31) katika kipindi cha XXL na kati ya vitu alivyozungumzia ni kuhusu tukio lake la kutoelewana na Elikem pamoja na sababu ya kupenda kuwa na ukaribu na visu na ina maana gani kwake.

“Mimi yani tokea nimekua mdogo mi nilikuwa naomba toys zile mi naomba mpira, bunduki ama kisu, sasa..sasa (akacheka) unajua ile tabia yani ya kuwa, sio kwamba nimetumia nimeshawahi kutumia sina kesi wala nini bana mi napenda hata nikizeeka ntakuwa na collectin ya visu….tuseme kama ukiwa nervous kuna vitu vile vya kuchezea kama mpira unao unajua ile…sasa mi nimezoea ile toka nakuwa nilikuwa nachezea kisu au nafanya hivi yani, ila sio kwamba violent wala nini sijawahi yani”.

Msikilize Nando hapa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents