Burudani

Makamua asaini mkataba mpya na MJ Records

Msanii wa kundi la Wakali Kwanza, Makamua amesaini mkataba mpya na MJ Records.

5defe034a9c311e3a0851240c301e87e_8

Makamua ameiambia Bongo5 kuwa ni jambo kubwa mno kuwa chini tena ya label hiyo.

“Nimesaini mkataba mpya wa kazi na MJ Records,” Makamua ameiambia Bongo5.

“Watu wamekuwa wakizungumzia chemistry yetu, nikaona huu ni wakati wa kurudi na kuonyesha kazi nzuri. Mimi najiamini kupita kawaida na bahati yangu najua ipo difference, so kila kitu ambacho kimepangwa na kina mipango dhabiti bila shika naamini kitafanikiwa vizuri,” ameongeza.

“Mimi sioni challenge kwenye huu muziki, kikubwa siwezi nikaacha muziki kwa sababu watu wengi nimewafanya waingie huku. Nikiacha watu ambao nimewavutia nao wanaweza wakaacha na generation nyingine ikafa.”

Makamua amesema anaamini kuwa ana nafasi kubwa ya kurudi tena kwenye chart.

“Kwanza wasanii wa sasa hivi wanafanya muziki wenye asili ya Kinageria,” anasema. “Mimi nitabaki kama Makamua. Kwenye huu muziki nafanya yangu na naona kabisa ya kufika mbali zaidi. Halafu pia kuna vitu vingi sana vinakuja. Kuna video nategemea kuachia inaitwa She is Gone, kuna wimbo nimefanya na Banana Zorro. Pia kuna project ambazo nimefanya kwa Fundi Samweli, kwahiyo mikakati ipo ya kumweka vizuri Makamua.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents