Habari
Marekani kuikabidhi kambi yake ya anga ya Bagram kwa Afghanistan
Jeshi la Marekani litakabidhi kambi yake kuu ya anga ya Bagram kwa vikosi vya Afghanistan, huku ikiendelea na kuondoa askari wake wa mwisho nchini humo.
Jeshi la Marekani litakabidhi kambi yake kuu ya anga ya Bagram kwa vikosi vya Afghanistan, huku ikiendelea na kuondoa askari wake wa mwisho nchini humo.
Kambi hiyo iliyojengwa na Wasovieti katika miaka ya 1980, ndiyo kubwa zaidi na ikitumiwa na vikosi vya Marekani na jumuia ya kujihami ya NATO huko Afghanistan.
Afisa usalama wa Afghanistan alisema makabidhiano hayo yanatarajiwa kufanyika katika siku 20 zijazo na wizara ya ulinzi imeunda kamati maalum za kuisimamia.
Kambi hiyo ambayo imekuwa ndiyo kituo kikuu cha kitaifa cha shughuli za jeshi la anga kwa miongo miwili iliyopita, kina gereza ambalo lilikuwa na maelfu ya wafungwa wa kundi la Taliban na wapiganaji wa jihadi.
Marekani tayari imekabidhi kambi nyingine kadhaa za kijeshi kwa vikosi vya Afghanistan kabla ya Mei 1, wakati ilipoanza kuharakisha mchakato wa kuwaondoa wanajeshi wake.