Michezo

Mavoko, Alikiba, Juma Nature na wengine kuchuana kwenye mechi ya soka na watangazaji wa EFM Jumapili hii

Rich Mavoko, Alikiba na Juma Nature ni miongoni mwa mastaa wa Bongo Flava watakaochuana kwenye mtanange wa soka Jumapili hii dhidi ya watangazaji wa kituo cha redio cha EFM.

Mechi

Mechi hiyo itachezwa Jumapili hii, June 26 kuanzia saa kumi jioni kwenye viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam.

Wasanii wengine watakaovaa jezi za Bongo Flava kwenye mechi hiyo ni pamoja na Tunda Man, M2thaP, Rich-One, Soggy Doggy, Kalapina, Jeby, Abdu Kiba, Inspector Haroun, H-Baba na KR Muller.

Wachezaji wa ziada ni pamoja na Suma G, Ally Com, Stamina, Afande Sele, Jay Moe, Mansu- Li na Young Killer huku makocha wa timu ya Bongo Flava wakiwa ni waheshimiwa Profesa Jay na Said Fella.

Kwa upande wa timu ya EFM, watakaokuwepo ni pamoja na Maulid Kitenge, Ibrahim Masoud (Maestro), Denis Ssebo, Omari Katanga na Swebe Santana.

“Lengo kubwa ni kukuza zaidi urafiki ambao upo kati yetu na kuimarisha mahusiano pamoja na kufahamiana zaidi,” wamesema EFM.

“Pia ni njia moja wapo ya kuimarisha afya zetu kama moja ya mazoezi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents