Picha

Mcheza mieleka Hulk Hogan akimbizwa hospitali baada ya mkono wake kuunguzwa na mlipuko wa radiator

Mcheza mieleka mkongwe Hulk Hogan ambaye jina lake si geni kwa wafuatiliaji wa mchezo wa mieleka, amejikuta akikimbizwa katika chumba cha dharula cha hospitali ya Florida Jumapili (May 26) baada ya mkono wake wa kushoto kujeruhiwa vibaya na moto uliotokana na mlipuko wa radiator katika boti yake.

hulk hogan

Hogan mwenye miaka 59 alitoa taarifa kwa fans wake kupitia mtandao wa kijamii twitter na kupost picha zinazoonyesha mkono ulivyoungua na moto na kuumia vibaya.

Tweet ya kwanza ya mkongwe huyo wa mieleka aliyoituma akiwa anasubiri kupata huduma ya kwanza hospitalini hapo ilisema “I [am] at the ER [Emergency Room] now at Tampa General Hospital,” ikifuatiwa na tweet nyingine iliyoambatana na picha moja inayoonyesha mkono ulioumia.

hogan 1

Nayo ilifuatiwa na tweet nyingine yenye picha mbili zingine na kuwashirikisha wasomaji maumivu aliyonayo kwa njia ya maandishi “Double Ouch,” na “Triple Ouch!” na zingine zilikuwa zikionesha wakati daktari anampa huduma ya matibabu.

hogan 2

hogan 5

Hata hivyo Hogan hakutoa maelezo zaidi ya nini kilisababisha mlipuko huo wa radiator katika boti yake.

Get well soon strong man!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents