Habari

Amini Usiamini: King wa Rap Kenya, Collo aja na ngoma ya lingala! ‘KUDYAMBO’

Moja ya sifa za mwanamuziki wa kweli ni pamoja na uwezo wa kubadilika katika kazi zake, kitu ambacho rapper aliyejipa ufalme wa rap Kenya Collo ameuonesha katika ‘surprise’ ya wimbo wake mpya wenye mahadhi ya lingala, yes sijakosea nimesema lingala!

collo n fetty

Hip Hop na lingala ni aina mbili tofauti sana za muziki japo hata lingala ina rap lakini sio kama ya hip hop, hivyo msanii anayefanya hip hop anapoamua ku-switch na kufanya ‘pure’ lingala na akaifanya vizuri sana anastahili heshima sababu huo si uwezo wa kubeza.

Ukiusikiliza wimbo huo mpya unaoitwa ‘KUDYAMBO’, unaweza usiamini kwa haraka kama huyu ndie yule Collo wa hit songs za hip hop kama King wa rap, Kuwa mpole, na collabo yake na P-Unit You guy, ameuvaa uhalisia wa lingala kama ndio genre yake ya siku zote.

Kwa mujibu wa mtandao wa Ghafla maandalizi ya video ya ‘Kudyambo’ yameanza ambapo Collo jana alitangaza shindano la kucheza la online kwa dancers wenye vipaji nchini Kenya, kuweza kutuma vipande vya video zao zenye choreography za wimbo huo kupitia Youtube, na makundi matatu yatakayomridhisha kiuwezo yatapata nafasi ya kushiriki katika video hiyo inayotegemewa kutoka July mwaka huu.

Well done man that’s what we call talent! You nailed “Kudyambo”!

Sikiliza hapa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents