Burudani

Miamala ya huduma ya M-Pesa yarahisishwa zaidi

Wateja wa mtandao wa mawasiliano wa Vodacom Tanzania Plc, kuanzia leo wataanza kunufaika na programu mpya na ya kisasa zaidi katika kufanya miamala yao kupitia huduma ya M-Pesa ambayo itawezesha watumiaji wa huduma hii wenye simu za intanenti kuifurahia zaidi kwa kuwa imerahisishwa na kuboreshwa zaidi.

Programu hii inawezesha watumiaji wa huduma ya M-Pesa kufanya miamala kwa haraka bila kufuata mlolongo mrefu wa programu ya awali – kwa mfano mtumiaji anaweza kuangalia akiba ya salio lake kwa kubonyeza mara moja maelekezo ya kupata huduma hii bila gharama yoyote. Pia programu hii imekuja na mfumo wa kufanya miamala ya malipo kwa teknolojia ya kisasa na haraka inayomrahisishia maisha mtumiaji.

Katika programu hii mpya pia inawezesha mteja kuona jina la wakala au jina la kampuni au biashara kabla ya kutoa au kutuma hususani katika miamala ya kulipa kwa kutumia huduma ya Lipa kwa M-Pesa.

Mkurugenzi wa huduma za biashara kwa njia ya mtandao wa Vodacom Tanzania Plc, Sitoyo Lopokoiyit,amesema kuwa programu hii imezinduliwa rasmi leo baada ya kufanyiwa utafiti katika soko na kujiridhisha kuwa italeta mapinduzi ya matumizi ya kufanya miamala ya fedha kwa M-Pesa kwa kuifanya kuwa rahisi zaidi kwa watumiaji hususani wanaotumia simu za intanenti (Smart Phones).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents