Burudani

Mike T atoa ofa ya video 10 kwa wasanii wachanga

Rapper Mike Tee ambaye pia ni mtayarishaji wa video za muziki chini ya kampuni ya Showbiz Defined, ameweka wazi mkakati wake wa kuwasaidia wasanii chipukizi.

Mike

Mike Tee ameiambia E-Newz ya EATV kuwa ameamua kutoa ofa ya kufanya video 10 kwa wale watakaokuwa na kazi nzuri.

Alisema zoezi hilo litaendeshwa mpaka tarehe 15 mwezi huu na ndani ya kipindi hicho wasanii watakuwa wakituma rekodi zao pamoja na taarifa zao muhimu kupitia mawasiliano ambayo ameyaweka katika ukurasa wake wa Facebook. Hii ni sehemu ya mkakati wa msanii huyo kuendelea kuwasaidia wasanii walio chini akiwa pia na mpango wa kusambaza kazi za wasanii wengine mitaani kama njia ya kuwasaidia kusikika kwa mashabiki wao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents