Burudani

Mike T kutoa documentary ya JWTZ itakayoshirikisha wasanii kuelimisha jamii

Baada ya kuongoza video ya wimbo wa ‘JWTZ’ wa Profesa Jay, Juma Nature na Jay Mo, Mike T amesema kitakachofuata baada ya video hiyo ni documentary kuhusu jeshi hilo.

MIKE TEE 1
Mike Tee,Proffesor Jay ,Jay Mo,Juma Nature pamoja na wanajeshi wa JWTZ

Mike T amesema maandalizi ya kazi hiyo yameanza vizuri ingawa wanapata changamoto kadhaa.

“Project inahusu kuelimisha jamii juu ya jeshi la JWTZ,watu wanatakiwa watambue mchango wa jeshi hili ndani ya nchi na nje ambapo mara nyingi jeshi letu limekuwa likienda kupambana na kusaidia nchi mbambali za Afrika,” ameiambia Bongo5. “Kwahiyo Watanzania wengi wamekuwa wavivu kusoma historia ya nchi yao,tukaona kupitia muziki tunaweza kuelimisha watu wa rika zote, kutambua mchango wa JWTZ hapa nchini na Afrika nzima. Baada ya video ambayo imetoka hivi karibuni,mpango unaofuata kwasasa tunaandaa documentary ambayo itakuwa inaonyesha matukio mbalimbali ya kihistoria ili watu waweze kutambua jeshi lao vizuri.Tumekumbana na changamoto nyingi na wengine wamefikia hatua ya kutuvunja moyo,unajua kuna kamanda wa kikosi cha hapa Mwenge ambaye alikuwa anatusimamia kwasasa amehamia Arusha kwahiyo yule ndiyo aliyekuwa anasimamia mambo mengi,sasa huyu aliyekuja duh kuna mambo ya malipo kwa baadhi ya wasanii hayaendi sawa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents