Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya urembo (Miss
Earth 2008), Miriam Odemba ameibuka mshindi wa pili (Miss Air 2008) katika fainali za
mashindano hayo zilizofanyikia jana nchini Ufilipino.
Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya urembo (Miss
Earth 2008), Miriam Odemba ameibuka mshindi wa pili (Miss Air 2008) katika fainali za
mashindano hayo zilizofanyikia jana katika ukumbi wa Clark Expo
Ampitheater mjini Pampanga, Ufilipino.
Mshindi wa kwanza ni Karla Paula Henry kutoka Ufilipino
huku nafasi ya tatu ikienda kwa Miss Mexico Abigail Elizalde. Mshindi wa
nne ni Miss Brazil, Tatiene Alvez.
Jumla ya washiriki 84 walishiriki
shindano hilo. Bongo5 inatoa hongera nyingi kwa Miriam Odemba kwa kuwakilisha nchi yetu na kutufikisha matawi ya juu kabisa! Big up!!