Michezo

Mkutano Mkuu wa Mwaka wa FIFA kufanyika Tanzania

Tanzania yateuliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Mwaka wa FIFA utaoshirikisha mataifa 19 na kufanyika Februari 22 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa mkutano huo, Rais wa FIFA Gianni Infantino, Katibu Mkuu wa FIFA, Fatma Samba Diouf Samoura na Sekretarieti ya FIFA pamoja na rais wa CAF, Ahmad Ahmad na Sekreterieti yake, ni miongoni mwa wageni wa ngazi ya juu watakaohudhuria.

Agenda kadhaa zitakazojadiliwa ni pamoja na utoaji wa Fedha za FIFA kwaajili ya maendeleo ya mchezo wa soka, changamoto za usajili wa wachezaji kwa kutumia mtandao yaani TRANSFER MATCHING SYSTEM na kalenda ya kimataifa ya FIFA.

Baadhi ya nchi zitakazoshiriki katika mkutano huo ni Bahran, Saudi Arabia, Palestina, Algeria, , Ivory Coast, Tunisia, Mali na Niger.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents