Burudani

Morocco: Rapper, Gnawi ahukumiwa kwenda jela kwa kosa la kuwatusi Polisi

Rapper Mohamed Mounir maarufu ‘Gnawi’ amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kutukana Polisi kupitia kipande cha video alichoposti kwenye mitandao ya kijamii.

Image result for Gnawi

Hata hivyo rapper huyo mwenye umri wa miaka 31, inadaiwa kuwa kukamatwa kwake kumechochewa zaidi na aina ya kazi zake za muziki, hata baada ya kuachia wimbo wake mpya ujilikanao kama “Aach al Chaab,” aliyowashirikisha Lz3er na Weld L’Griya ambao unazungumzia vitendo vya rushwa Serikalini.

Serikali imekanusha kukamatwa na rapper huyo hakuhusiani na wimbo wake huo bali ni kutokana na video hiyo iliyosambaa mitandaoni inayotusi polisi.

Image result for Gnawi

Kwa mujibu wa Al Jazeera reports. Wimbo huo mpya aliyoupa jina la “Aach al Chaab,” ukiwa na maana ya kuwataka watu kuishi kwa muda mrefu ama kuwatakia maisha marefu umetanabaisha wazi wazi maswala ya ukosoaji rushwa, ukosefu wa ajira na unyanyasaji serikalini. Wimbo huo mpaka umekuwa gumzo nchini Morocco na ukizidi kupata watazamaji kupitia You Tube.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents