Burudani

Msanii wa Kenya adhamini mradi wa maji kwenye shule wenye thamani ya shilingi milioni 36 za Tanzania

Msanii wa muziki wa Kenya, Esther Akoth aka Akothee anafahamika kwa miradi yake ya kusaidia jamii.

20150319053124 (2)
Akothee (katikati) akiwa na walimu wa shule ya sekondari ya St. Alberts Ulanda Girls iliyopo Migori, Kenya

Hivi karibuni, Akothee amejitolea kudhamini mradi wa maji kwenye shule ya wasichana iliyopo kwenye kaunti ya Migori nchini Kenya.

20150319053124

Shule hiyo iitwayo St. Alberts Ulanda Girls imekuwa ikikabiliwa na tatizo sugu la maji katika miaka yake yote tangu kuanzishwa japo ni miongoni mwa shule zinazofanya vyema kitaifa.

20150319053124 (4)

Akiongea kwenye mkutano wa shule hiyo, Akothee aliahidi kugharamikia kutengenezwa kwa mabomba ya maji katika shule hiyo ambapo mradi mzima unakadiriwa kugharimu shilingi milioni 2 za Kenya, sawa na shilingi milioni 36 za Tanzania.

20150319053124 (1)
Akothee akipata chakula na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo

Alisema hadi mwisho wa mwaka huu mradi huo utakuwa umekamilika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents