Habari

Muigizaji Van Vicker wa Ghana aamua kuingia kwenye muziki

Muigizaji wa Ghana, Van Vicker ambaye mwaka jana mwishoni amefanya filamu na staa wa Bongo Wema Sepetu, ameamua kutupa karata yake kwenye muziki.

Van Vicker 1
Wema Sepetu na Van Vicker wa Ghana

Akizungumza kwenye mahojiano ya hivi karibuni, Vicker ambaye pia ni producer na muongozaji wa filamu amesema kuwa ameamua kujaribu kuingia kwenye muziki kwasababu ameshafanya mengi kwenye tasnia ya filamu, hivyo ameona aweke mchango wake kwenye kiwanda cha muziki pia.

“I have chosen music now because I think I have done much for the movie industry, with my Van Vicker training facility; being a producer and a director as well- so time to contribute to the music industry as well.”

Van.v

Alipoulizwa aina gani ya muziki anayotaka kujihusisha nayo alisema mtindo wowote ambao unavutia soko la kimataifa.

“Any genre that can catch the international eye, ‘I am looking at discovering a talent for the international market, it doesn’t matter if is hip-life, gospel, raggae, etc, what matters is real talent.”

Source: Ghana Vibes

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents