HabariUncategorized

Mwanafunzi alitaka kutoboa bomu akidhani chuma chakavu – RPC Kagera

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani kagera Agustino Olomi amesema chanzo cha wanafunzi kupoteza maisha na kujeruhiwa kwa bomu ni kutokana na mwanafunzi kuokota bomu hilo akidhani chuma chakavu ili aweze kwenda kuuza.

Picha hii sio ya bomu husika

Kamanda huyo amewaambia waandishi kuwa katika kijiji hicho kumekuwa na tabia ya kuuza vyuma chakavu ambapo mnunuzi huwa akiwapatia malipo ya madaftari.

Kwa upande wa Kamanda wa Kikosi cha kulinda mipaka cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wilaya ya Ngara Meja TR Mutaguzwa amesema Bomu hilo lilikuwa na vipande 36 na lingelipukia ndani ya darasa lingeleta athari zaidi .

Mlipuko wa bomu hilo umesababisha vifo vya wanafunzi tisa huku wengine wajeruhiwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents