Burudani

Nay wa Mitego kuvunja ukimya na ‘Nyumbani Kwetu’

Rapper Nay wa Mitego amesema anatarajia kuachia wimbo mpya uitwao ‘Nyumbani Kwetu’ ambapo amedai watu watashangaa jinsi alivyobadilika kwenye uimbaji.

Nay wa Mitego

Nay amedai kuwa wimbo huo utatoka ukiwa pamoja na video.

“Wimbo unaitwa Nyumbani Kwetu, kwani muziki fulani wa tofauti ambao sijawahi kufanya. Pia hii ni surprise kwa mashabiki wangu wote ambao wanapenda muziki wangu na sidhani kama kuna mtu aliwahi kufikiria kama nitafanya muziki wa aina hii,” rapper huyo alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.

“Watu wakae tayari nimeshaanza kushoot video hata kabla ya uchaguzi kUisha lakini nashukuru Mungu leo ndio naingia tena location kwa mara ya mwisho. Baada ya hapo nadhani wiki ijayo Jumatano ngoma itatoka.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents