Burudani

Ndoa ya Kanye west na Kim kardashian matatani, mbioni kupeana talaka (+ Video)

Mlimbwende wa Marekani Kimberly Noel Kardashian West alimaarufu Kim Kardashian na mume wake rapper Kanye Omari West alimaarufu  Kanye West wamekuwa wakipata ushauri wa ndoa yao,lakini mtandao wa TMZ nchini humo umeripoti kwamba kwa suala la wawili hao kutengana limekuwepo kwa muda mrefu lakini hawajakata tamaa.

Vyanzo kadhaa vya habari vimeripoti taarifa zinazowahusu wawili hao vimeuambia mtandao huo nchini Marekani , kwamba ndoa hiyo ilikuwa katika matatizo makubwa katika nusu ya mwisho wa mwaka 2020.

Habari zinasema kwamba Kim alikuwa tayari kuomba talaka katika tukio moja lakini kwasababu Kanye alikuwa anakumbwa na tatizo la kiakili akaona kwamba sio vyema kuchukua hatua hiyo wakati ambapo hali ya mume wake sio nzuri.

Wamekuwa wakiishi kwa kutengana kwa miezi kadhaa huku Kanye West akitumikia wakati wake mwingi katika eneo la Wyoming naye Kim Kardashian akiwa katika eneo la Calabasas na watoto.

Wote wamekuwa katika harakati za kazi zao na hawakuangazia kufanya uamuzi wowote wa mwisho wa kutangaza kuachana ama kuongelea suala hilo ambalo linagonga vichwa vya habari kwa miezi kadhaa sasa.

Bofya hapa:

https://www.instagram.com/tv/CJvD3puhFId/

https://www.instagram.com/tv/CJvD3puhFId/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents