Burudani

Nedy Music ataja sababu ya Ommy Dimpoz kutomweka wazi mpenzi wake

Msanii Nedy Music amefunguka sababu ya bosi wake wa lebo ya PKP, Ommy Dimpoz kutomuweka wazi mpenzi wake kwa mashabiki.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, muimbaji huyo amedai kuwa unapokuwa kwenye mahusiano si lazima umpost mpenzi wako mitandaoni.

“Unajua mahusiano ni mambo ambayo hayaingiliwi, hivyo isiletwe picha kuwa ni lazima unapokuwa na mwanamke au unapokuwa kwenye mahusiano lazima umposti kwenye mitando ya jamii. Mimi leo kioo cha jamii nikimposti mwanamke niliyenaye kwenye mahusiano halafu kesho nikagombana naye, nikawa na mwingine tena lazima mashabiki watataka nimposti. Sasa nikimfanya hivyo nitakuwa naleta picha gani kwa mashabiki na jamii kiujumla,” amesema Nedy.

Kwa sasa msanii huyo anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Rudi’ aliomshirikisha Christian Bella.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents