Wasanii mbalimbali wa kike nchini wameungana pamoja kurekodi wimbo uitwao ‘Simama Nami’ maalum kwaajili ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya albino vinavyoendelea nchini. Wimbo umeandikwa na Barnaba.
Wasanii walioshiriki ni pamoja na Keisha, Mwasiti, Linah, Khadija Nito, Grace Matata, Shilole, Kajala, Wolper,Shamsa Ford, Irene Uwoya na Zamaradi Mketema. Wimbo umefanyika katika studio za Switch Records.