Uncategorized

Ole Gunnar Solskjaer awasili Manchester United, mbivu au mbichi kuhusu kukabidhiwa timu kujulikana wiki hii

Ole Gunnar Solskjaer ameonekana akiwasili Carrington kwaajili ya majukumu yake ya kila siku, huku akitarajia kupewa mkataba wa kudumu ndani ya Manchester United. 

Kocha huyo anarudi United akitoka kwenye mapumziko wakati ambao baadhi ya wachezaji walikuwa wakizitumikia timu zao za taifa na sasa yupo tayari kukiandaa kikosi chake kwaajili ya kuvaana na Watford siku ya Jumamosi.  

Inaaminika kuwa Solskjaer atapewa Mkataba wa kudumu wa kuifundisha Manchester United kabla ya mwisho wa wiki hii.

Kocha huyo mwenye umri wa mika 46, raia wa Norway mpaka sasa ameweka rekodi bora kabisa ya kushinda jumla ya michezo 14 kati ya 19 aliyosimamia klabu hiyo tangu kuchukua nafasi ya Jose Mourinho mwezi Desemba. 

United imezidiwa pointi mbili na Arsenal yenye alama 60 inayoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Premier League huku ikitarajiwa kukutana na Barcelona hatua ya robo fainali ya Champions League mwezi ujao. 

Ukiachiambali kocha huyo wapo baadhi ya nyota wa timu hiyo ambao wamewasili akiwemo Marcus Rashford na Jesse Lingard.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents