Burudani
Picha: Mwili wa Papa Wemba wawasili Kongo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi
Mwili wa marehemu, Papa Wemba umewasili nyumbani kwao Kongo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.
Muimbaji huyo nguli alianguka jukwaani weekend iliyopita na kufariki wakati akiwatumbuiza maelfu ya mashabiki wake waliojitokeza katika tamasha la muziki mjini Abidjan Ivory Coast.
Mwanamuziki huyo ambaye ametajwa kuwa mmoja ya waanzilishi wa muziki wa kizazi kipya cha Soukous anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne baada ya mwili huo kuwekwa katika uwanja wa mpira kwa raia kutoa heshima zao za mwisho
Picha: Epa,Mpasho