Burudani

Polisi wavamia nyumba ya Lil Wayne na kuchukua mali kutokana na deni la kukodi ndege binafsi

Polisi walivamia nyumba ya Lil Wayne huko Miami Beach Jumanne hii na kuchukua mali mbalimbali kutokana na deni alilonalo rapper huyo baada ya kukodi ndege binafsi na kushindwa kulipa.

url

Kwa mujibu wa TMZ, polisi walipofika nyumbani kwa Weezy, walinzi waliwauzia kuingia ndani. Maofisa walieleza kuwa walienda hapo kukamata vitu mbalimbali kwakuwa Wayne hajalipa deni lake la dola milioni 2 za kukodi ndege kutoka kwenye kampuni ya Signature Group.

Kampuni hiyo ilimshtaki Weezy kwa kushindwa kulipa gharama hizo kwa miaka miwili. Pia inataka ilipwe $200,000 kama gharama za mwanasheria.

Mahakama iliwaruhusu maofisa kuvunja makufuli ya nyumba hiyo na kushikilia mali mbalimbali. Wayne hakuwepo nyumbani muda huo.

Alionekana kwenye club ya usiku ya huko Los Angeles Jumatatu hii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents