Burudani

Profesa Jay afungua website yake rasmi (official website)

Profesa Jay ameingia kwenye list ya wasanii wa Tanzania ambao wameona haja na umuhimu wa kufungua website zao, kwa kuanzisha website yake www.profesajay.com ambayo itakuwa inaweka matukio mbalimbali yanayohusu kazi zake, na kurahisisha upatikanaji wa habari zake, nyimbo pamoja na video zake.

profesa-Jay

“Nimeamua kuwa na website yangu kuzidi kujitengeneza, kujipackage na mtu aweze kukufikia kirahisi… Nimeona value yangu na nimeona wapi nilikosea, kwa muda mrefu watu wemekuwa wakiulizia website, kazi zangu watazipata wapi, wapi muziki wangu, wapi shows zangu…So kila kitu ntakachokuwa nafanya kitakuwa kinapatikana kwenye website yangu.”
Alisema Profesa Jay kupitia Bongo Dot Home ya Times Fm.

Wasanii wengi ambao walitangulia fungua website zao ni pamoja na AY, C-Pwaa, Mwana FA, Diamond Platnumz, Dully Sykes na wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents