Burudani

Rita Paulsen: Bongo Star Search inarudi kwa kishindo

Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark na Jaji kiongozi wa mashindano ya kusaka vipaji vya muziki, maarufu BSS, Rita Paulsen amewataka mashabiki na wapenda muziki kuondoa hofu akieleza kuwa mashindano hayo hayajafa.

10460318_795258267191563_5051762902044579865_n

Mashindano ya BSS mwaka jana hayakufanyika na hali hiyo ilizua hofu miongoni mwa mashabiki kwamba huenda mashindano hayo yamekufa.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi jana, Rita alisema kuwa licha ya shindano hilo kuchelewa kuanza katika msimu huu, litafanyika na kwamba mipango inakamilishwa.

“Najua Watanzania wana hamu ya kushuhudia msimu mwingine wa ukianza. BSS ni mapinduzi hasa kwa vijana nayo hayaishi kwa siku moja, lakini kwa sasa kuna mambo tunayaweka sawa, hadi mwishoni mwa Februari mipango itakuwa imekamilika,” alisema Rita.

Pamoja na BSS, Madam Rita anatarajiwa kuja na kipindi chake cha runinga, The Rita Paulsen Show.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents