Burudani

Roberto wa ‘Amarula’ awataja wasanii wa Tanzania aliofanya nao collabo

Hit maker wa ‘Amarula’, Roberto kutoka Zambia amewataja wasanii wa Tanzania ambao tayari amefanya nao kazi na ambao anatarajia kufanya nao collabo.

Roberto

Roberto ambaye amekuja Tanzania kwaajili ya show leo Dec 11 jijini Dar, amesema amefanya collabo na Vanessa Mdee na wanatarajia kuitoa mwakani.

“Wimbo niliofanya na Vanessa umekamilika, sasa tunafanyia kazi mipango ya kuitoa unajua nina mheshimu Vanessa na muziki wake na yeye ananiheshimu pia hivyo tulikubaliana tusiitoe hivi hivi tu tuwe na mpango mkakati wa jinsi wa kuitoa.” Alisema Roberto kupitia Ayo Tv.

Amemtaja pia Shetta kuwa ana mpango wa kufanya naye kazi pamoja na msanii mpya kutoka Rock City, Fred Swag.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents