Michezo

Serikali yaja na mpango wa mabwawa ya kuogelea

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison amesema Serikali imeahidi kujenga mabwawa 10 ya kisasa ya kuogelea kwa ajili ya kuendeleza mchezo huo hapa nchini.

Waziri, Mwakyembe ameyasema hayo katika uzinduzi wa mashindano ya kanda ya tatu ya Afrika yanayoandelea kwenye bwawa la shule ya Kimataifa ya Heaven of Peace hapo jana

Waziri huyo amesema kuwa wamefarijika sana na vipaji vya waogeleaji wa Tanzania katika mashindano  hayo ambayo yameshirikisha jumla ya nchi sita ikiwemo ya Tanzania. Nchi nyingine ni Kenya, Uganda, Sudani, Afrika Kusini na Zambia.

“Nimesikitika sana kusikia kuwa kuna wawekezaji walikuja hapa kutaka kujenga bwawa la kuogelea kwa ajili ya maendeleo ya mchezo huu na kukatishwa tamaa na baadhi ya watendaji wa wizara yangu,” amesema Mwakyembe.

Mwakyembe ameongeza “Nawaahidi kulishughulikia suala hili kabla ya mwisho wa mwezi huu, nitakutana na Waziri wa Tamisemi na kuona ugumu upo wapi hasa kwa shule maarufu ya msingi ya Oysterbay ambayo ilikuwa iwe ya kwanza kujengewa bwawa la kisasa la kuogelea.”

Katibu Mkuu wa chama cha kuogelea hapa nchini (TSA), Ramadhan Namkoveka ameipongeza Serikali kwa kutoa ahadi hiyo.

“Tumefarijika na ahadi ya serikali kwakuwa tumekuwa tukiangaikia suala la kupata bwawa la kisasa la kuogelea miaka mingi.” amesema Namkoveka.

Namkoveka pia aliwapongeza wachezaji wa Tanzania kwa kuanza kwa vishindi mashindano hayo na kutwaa medali 21 ambapo, nane ni za dhahabu. Waogeleaji, Sonia Tumiotto na Natalie Sanford kila mmoja alitwaa medali mbili za dhahabu katika mashindano hayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents