Burudani

Shaa asema 2015 ataendelea kufanya muziki kama ‘Sugua Gaga’ baada ya wimbo huo kumpa mafanikio

Mwimbaji Shaa amesema kuwa baada ya ‘Sugua Gaga’ kufanikiwa kumtambulisha kimataifa mwaka jana (2014), ana mpango wa kuendelea kufanya nyimbo za aina hiyo mwaka huu.

Shaa sugua gaga

Shaa ambaye video ya Sugua Gaga ilifanikiwa kuwa video ya msanii wa Tanzania iliyotazamwa zaidi mwaka jana kwenye mtandao wa Youtube, amekiri kuwa hakutarajia mafanikio hayo wakati anautoa wimbo huo. Ameongeza kuwa wasanii wengi wa Afrika Mashariki wamemshauri anedelee kufanya muziki wa aina hiyo.

“Mwaka jana kweli nilivyotoa Sugua Gaga na Subira nilikuwa nikiangalia zaidi soko la hapa nyumbani, sikutegemea kwamba muziki huo huo unaweza akanivukisha boda, ni mara yangu ya kwanza kufanya single yangu kubwa ambayo imewahi kupata hits zaidi ya milioni 15 kwenye Youtube, ndio video iliyotazamwa zaidi kwa mwaka jana 2014.” Shaa aliiambia E-Newz ya EATV.

“Hata navyovuka mipaka Kenya nao wanasema hivyo hivyo si tunamfahamu Shaa wa Sugua Gaga, Uganda nimekutana na Chameleone na Maurice wananiambia dada Sugua Gaga ndio habari ya mjini. Kwahiyo we unaweza ukakaa ukafikiri zile za kishua ndio zilikuwa zinanitambulisha nini kumbe hapana boss kumbe ni zile za nyumbani zaidi. Kwa hiyo kwa mwaka huu nikasema nitajipanga hivyo hivyo nitaangalia kile kitu ambacho kimewavutia zaidi mashabiki wangu ndo nitaendelea line hiyo hiyo.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents