Burudani

Sifanyi collabo za nje sababu sioni kama zina faida yoyote kwenye muziki wangu – Mwana FA

Sio ngumu kwa Mwana FA kupata collabo za wasanii wa nje ya Tanzania kama akiamua, kwasababu rafiki yake wa karibu AY ana connection na wasanii wengi wa Afrika na nje ya Afrika. Lakini Binamu hana mpango huo kwasasabu haoni kama zina faida yoyote kwenye muziki wake.

FA Kili

“Nafikiri nawafanyia muziki watu wangu wa hapa,” Mwana FA ameiambia 255 ya Clouds Fm. “Na ilivyo ni kwamba ukiangalia mi naandika zaidi AY anafanya ma-fleva zaidi, kwahiyo anaweza kufanya muziki ambao lugha mtu haielewi lakini aka bang nao. Mi nafanya conscious ile hata kila mtu anayeniskiliza aelewe nini nachosema, na lugha ninayotumia inafanya watu wanaoweza kuskiliza muziki wangu ukawashika moja kwa moja ni watu wanoongea Kiswahili kwahiyo sioni sababu ya kwanini nijihangaishe.”

Binamu ameongeza kuwa ikitokea kuna msanii wa nje akahitaji kufanya naye collabo atakuwa tayari kufanya hivyo, lakini sio yeye kutaka kufanya collabo na msanii wa nje.

“Kama ntatoka kufanya featuring nje ya nchi basi nataka nitoke kama msanii aliyehitajika kutoka bongo sio kwasababu mimi nataka kufanya tu sioni kama inafaida kwenye muziki wangu.” alimaliza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents