Burudani

Mnakosea mnaponiita mimi ni msanii wa Bongo Flava – Christian Bella (Video)

Christian Bella amesema watu wanakosea kumuita msanii wa Bongo Flava.

Tatizo hilo limesababisha hadi kwenye tuzo za KTMA 2015 asiwekwe kwenye kipengele chochote cha muziki wa bendi, kitu ambacho amesema hajakifurahia.

“Mimi sipo kwenye Bongo Flava, mimi napiga muziki, unajua ndio maana wasanii wengi wanapotea kwasababu wanashindwa kusoma ramani,” ameiambia Bongo5.

“Kama umeiona Taarab inakiki lazima utafute flavor ambayo itakufanya uingie humo humo. Mimi naangalia upepo unavyokwenda. Mimi sipigi Bongo Flava ila napiga muziki ambao watu wanaupenda.

Nikiona watu wanapenda Bongo Flava naangalia Diamond anaimba nini, kwanini watu wanampenda Diamond, naangalia watu wanapenda vitu gani, na mimi napiga kwa sauti ya Christian, haimaanishi mimi ni Bongo Flava,” alilisitiza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents