Burudani

Sitaki kuwa na meneja kwa sasa – Nuh Mziwanda

Nuh Mziwanda hataki meneja.

11242860_1641904692760686_468259681_n

Muimbaji huyo wa Hadithi anaamini kuwa mameneja wengi hawapo makini na kazi yao. Amesema wengi wanashindwa kujua nini wanatakiwa kufanya kwa wasanii wao.

“Mimi kama mimi suala la kuwa na meneja au menejimenti ni suala zuri lakini napenda nijipe muda,” muimbaji huyo aliiambia Planet Bongo EA Radio.

“Ukitaka meneja, unatakiwa upate meneja mzuri, meneja ambaye anaweza kusimamia kazi zako vizuri watu wakazielewa. Meneja ambaye anajua mimi siwezi kula bila nyimbo ya Nuh kufanya poa, mimi siwezi kula bila nyimbo ya Nuh kusambaa mtaani. Mimi siwezi kuwa meneja nakutegemea wewe, wewe unakuwa kama bosi.”

“Hapa Tanzania wapo mameneja wanaweza kufanya kazi vizuri lakini kwa upande wangu mimi ni suala ambalo nataka niende nalo taratibu ili nipate mtu anayefaa na atakayeweza kuniongoza vizuri. Ila kwa sasa nafanya kazi mwenyewe na changamoto nazipata kwa mfano nikiachia nyimbo nakuwa na vitu vingi vya kufanya. Nitaenda huku nitaenda huku, kama msanii nakuwa nachoka hata muda wa kukaa studio nashindwa kwa sababu ya kuzunguka huku na kule,” aliongeza Mziwanda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents