Burudani

Stamina kuachia albamu mpya Disemba, itakuwa na nyimbo 15

Rapper Stamina baada ya kufanya vizuri na albamu yake ya ‘Mt Uluguru’ anajipanga kuachia albamu mpya mwezi Disemba ambayo itakuwa na nyimbo 15.
Stamina2

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Stamina amesema tayari ameshamaliza kurekodi nyimbo zote za albamu hiyo na sasa ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya kutoka.

“Albamu mpya kwa sasa ipo jikoni kwa Rash Don, nimeshamaliza kurekodi na Disemba inaingia sokoni,” alisema Stamina. Nashukuru mungu hii ni tofauti ili iliyopita, mapaka sasa ninapozungumza na wewe tayari kuna wadhamini wamejitokeza kwa ajili ya usambazaji pamoja na kuandaa matamasha ya uzinduzi,”

Rapper huyo amesema nyimbo hizo 15 amefanya na maproducer tofauti tofauti ili kupata ladha tofauti katika kila wimbo.

Albamu iliyopita ya ‘Mt Uluguru’ iliuza nakala 9,000.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents