Michezo

Sure boy kutoka Azam atua Yanga, aandika ujumbe huu

Kupitia ukurasa wa Instagram wa klabu ya Yanga wameandika kuwa:- Zawadi ya mapema msimu huu wa Sikukuu kwa Wananchi. @sure8boy is now green & yellow🔰 Tunawatakia Kheri na Fanaka ya Sikukuu ya Christmas.

Lakini kupitia ukurasa wa Instagram wa Sure boy ameandika maneno haya:-

Assalam Alaykum,

Nitumie Fursa Hii Kushukuru Management, Technical Staff, Makocha, Viongozi, Mashabiki, Wachezaji Wenzangu Na Wafanyakazi Wote Wa @azamfcofficial Tuliofanya Kazi Kwa Pamoja Kwa Ushirikiano Kwa Kipindi Kirefu Sana.

Nyakati Za Huzuni, Majonzi Na Furaha Zote Tulisimama Pamoja Kuipigania Team Kwa Jasho Na Damu.

Nimeishi Kama MwanaFamilia Kwa Miaka Yote Hapo Klabuni, Nilikuja Nikiwa Kijana Mdogo Sana .

Naondoka Kutafuta Changamoto Mpya Nikiwa Nimepuvuka Kimwili Na Kiakili.

Mimi Ni Binaadamu Kama Kuna Sehemu Nimewakosea Naombeni Mnisamehe Na Mimi Pia Nimesamehe Kama Mlinikosea.

Asanteni Sana @azamfcofficial Nathamini Mchango Wenu Mkubwa Katika Maisha Na Career Yangu Kwa Ujumla.

SALUM ABUBAKAR SALUM

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents