Tragedy

Takriban watu 48 wauawa kwa risasi nchini Kenya, Al-Shabab watuhumiwa kuhusika

Takriban watu 48 wameuawa na wengine zaidi 25 kujeruhiwa kwa risasi baada ya watu zaidi ya 50 kushambulia majengo katika mji wa Mpeketoni uliopo pwani ya Kenya usiku wa kuamkia leo.

11

Wanamgambo hao walilenga hoteli mbili, benki na kituo cha polisi wakiwa na bunduki na bomu. Akiongea na shirika la Reuters, Mkuu wa jeshi la polisi la Kenya David Kimaiyo alisema hadi sasa hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

222
Miili ya watu waliouwa kwenye shambulio hilo

Kimaiyo alidai kuwa kundi la Al-Shabab huenda limehusika katika shambulio hilo. Hoteli na baa zinadaiwa zilikuwa zimejaa watu wakiangalia mechi za kombe la dunia kipindi watu hao walipovamia.

Kundi la AL-Shabaab liliapa kulipiza kisasi kwa kufanya mauaji katika ardhi ya Kenya baada ya majeshi ya nchi hiyo kwenda nchini Somalia mwaka 2011 kuwasaka wanamgambo hao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents