Habari

TANZIA: Kofi Annan afariki dunia

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan amefariki dunia leo Agosti 18, 2018 nchini Uswisi baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Mwanadiplomasia huyo kutoka Ghana, Annan amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80 huku akiwahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kati ya mwaka 1997 na 2006.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ametuma salamu za rambirambi baada ya kifo cha Annan huku akimwagia sifa kuwa alikuwa msimamizi elekezi wa mema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents