HabariMichezo

#TETESI Moloko kuelekea Singida FG

Inaarifiwa kuwa klabu ya Yanga imeanza mazungumzo na klabu ya Singida Fountain Gate juu ya kumwachia mchezaji wao Jesus Moloko kwenda kwa walima alizeti kwa mkopo wa muda wa miezi 6 katika dirisha hili dogo.

Moloko anatarajiwa kupunguzwa kwenye kikosi cha Wananchi ili kupisha nafasi ya wachezaji wa kigeni katika dirisha hili, mara baada ya utambulisho wa winga wa zamani wa Simba Augustine Okrah uliofanyika siku ya tarehe 31, 2023 akitokea klabu ya Bechem United ya Ghana.

Augustine Okrah akiwa na klabu ya Bechem United msimu katika Ligi kuu ya Ghana amefanikiwa kufunga magoli 9 akiwa kinara wa ufungaji katika mzunguko wa kwanza wa Ligi akiwa amefungana na Isaac Mintah kutoka Aduna Stars ya Ghana.

Je ni sahihi kwa Klabu ya Yanga kuachana na Moloko au nani ungependezwa kati ya wachezaji wa kigeni aweze kuachwa kwa ajili ya kuacha nafasi ya maingizo mapya?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents