Habari

Tutatafakari mkutano wetu na Marekani – Iran

Naibu Waziri wa Mambo ya nje wa Iran Abbas Araqchi amesema nchi yake haijafikia uamuzi lakini inayatafakari mapendekezo ya Umoja wa Ulaya juu ya kufanyika mkutano usio rasmi kati ya wanachama wa sasa wa mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 ambapo Marekani iliyojitoa kwenye mkataba huo pia itashiriki.

 

Iran na Marekani zimekuwa zikirushiana mpira kuhusu nani anapaswa kuchukua hatua ya kwanza ya kuyafufua mazungumzo juu ya mpango wa nyuklia wa Iran.

Image result for iran nuclear

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aliiondoa nchi yake kwenye mkataba huo na kuiwekea Iran vikwazo. Waziri wa Mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell anaweza kuanzisha hatua za mazungumzo hayo.

Wakati huo huo mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uangalizi wa Nguvu za Nyuklia (IAEA), Rafael Grossi, aliwasili mjini Tehran siku ya Jumamosi, wiki chache baada ya bunge la Iran kutangaza tarehe ya mwisho ya Februari 23 kwa Marekani kuiondolea vikwazo nchi hiyo vinginevyo itasitisha shughuli za ukaguzi wa shirika la IAEA nchini humo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents