Burudani

Tyga awatibua The Kardashians, wadai anachafua ‘brand’ yao

Familia ya The Kardashians imechukizwa na mwenendo wa rapper Tyga.

b1d7c953-1aa0-4b8d-9c3c-ce86924ea80b

Ni baada ya wiki hii jaji kuamrisha kukamatwa kwa rapper huyo mwenye uhusiano na mtoto wa familia hiyo, Kylie Jenner.

Vyanzo vimeiambia tovuti ya TMZ, kuwa baadhi ya wanafamilia hiyo wamemlaumu Tyga kwa kuwa mzembe kiasi cha kushindwa kutokea mahakamani, msala ulikoanzia.

Walimweleza kuwa itakuwa majanga kama atakuwa akiendesha gari na Kylie na kisha kukamatwa na polisi kama ilivyoamriwa. The Kardashians wanadaiwa kutopenda mambo hayo ya kihuni kwakuwa yanaharibu brand yao.

Tyga alishindwa kwenda mahakamani kwasababu alikuwa mapumzikoni na mpenzi wake Kylie aliyetimiza miaka 19, Jumatano hii. Inadaiwa kuwa tayari ameajiri mwanasheria kumtetea.

Tyga alishtakiwa na mwenye nyumba aliyokuwa amepanga anayemdai $480k. Alitakiwa kwenda mahakamani Jumanne ili kueleza kwanini ameshindwa kulipa deni hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents