Habari

Ujumbe wa Dr. Mengi kwa Rais Magufuli

Mwenyekiti wa IPP Dr. Reginald Mengi‏ amedaiwa kumtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa makini na baadhi ya watu.

Dr. Mengi akiwa na Rais Magufuli katika moja ya tukio la hivi karibuni

Mengi amedai katika maisha kuna wakati unaweza kuona upo pamoja na watu fulani kumbe sio kama unavyofikiria.

Waogope watu wanaokuambia eti wako nyuma yako. Mara nyingi ukigeuka nyuma hawapo @ MagufuliJP” alitweet Dr. Reginald Mengi‏ Jumatatu hii.

Kauli hiyo haikujulikana wazi inamaanisha nini moja kwa moja ila wadau wa mambo wanadai hatua hiyo imekuja kutoka na sakata la ndege ya Bombadier ambayo inadaiwa kushikiliwa nchini Canada.

Taarifa hiyo ilidai kuwa kuna wanasheria wa Kampuni fulani ya Nchini Italia ikishirikiana na baadhi ya watu kutoka Tanzania, waliweka zuio la ununuzi wa Ndege hiyo kwa maelezo kwamba wanakamata mali hiyo ya serikali kwa kuwa kuna Kampuni inayoidai Serikali ya Tanzania.

Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali Jumamosi hii iliuufahamisha Umma kuwa mgogoro huo upo ila kimsingi ni mgogoro ambao umetengenezwa na Watanzania wenzetu ambao kwa bahati mbaya sana wameweka maslahi ya kisiasa na ya binafsi mbele zaidi ya maslahi ya Taifa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents