Michezo

USAJILI: Deogratius Munishi ‘Dida’ aipa mkono wa kwaheri Yanga SC.

Kocha wa makipa wa klabu ya Yanga SC, Juma Pondamali (Mensah) amethibitisha timu hiyo kuachana na golikipa wake mahiri Deogratius Bonventure Munishi (Dida).

Kocha wa makipa wa klabu ya Yanga SC Juma Pondamali (Mensah)

Pondamali amesema Dida amegoma kuingia mkataba na Yanga kwa madai kuwa anaenda kufanya majaribio nje ya nchi.

Mcheza soka huyo mkongwe amesema tayari wamemnasa kipa wa klabu ya African Lyon atakayesaidiana na Beno Kakolanya na kipa mwingine mdogo.

Golikipa, Deogratius Bonventure Munishi (Dida) .

Kupitia mahojiano na Radio One Pondamali amesema kuwa Dida alitoa sharti la kuongeza mkataba mara baada ya kumaliza majaribio yake nje ya nchi kitu ambacho Yanga imedai haina muda wa kusubiri jambo hilo.

Siku za hivi karibu mlindalango huyo amekuwa akihusishwa kuwindwa na klabu ya Singida United.

By Hamza fumo

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents