MichezoUncategorized

USAJILI: Mkude awaweka ‘roho juu’ viongozi wa Simba SC

Nahodha wa klabu ya Simba SC, Jonas Mkude bado ameiweka klabu yake njia panda baada ya taarifa za kuihama klabu hiyo kuendelea kusambaa kila kona.


Jonas Mkude

Taarifa za ndani kutoka klabuni hapo zimeeleza Mkude bado hajafikia muafaka wa kuongeza mkataba na wekundu hao wa Msimbazi kitu ambacho kinawaweka roho juu mashabiki na viongozi wa klabu hiyo.

Bongo Five ikiongea na moja ya Wadau wa karibu wa timu hiyo amesema kwa sasa bado kuna vitu vidogo vidogo ambavyo mkude anavihitaji na tukisha malizana nae atasalia klabuni hapo.

“Hakuna wa kumchukua Mkude, sisi na Mkude, tuko vizuri na huenda akasaini ndani ya siku mbili zijazo kwani kuna vitu vichache anavitaka kwenye mkataba wake mpya hakuna shaka atasalia hapa,” amesema moja ya Mdau mkubwa wa kamati ya usajili ya Klabu ya Simba ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Mvutano huo umekuja baada ya taarifa za Ibrahim Ajibu kuhama klabuni hapo na kujiunga na Klabu ya Yanga huku kukiwa na taarifa nyingine za beki kisiki wa Simba, Abdi Banda naye akitaka kuihama Klabu ya Simba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents