Burudani

Vanessa Mdee aelezea show ya ‘Gidi Culture Festival’ ya Nigeria ilivyompa mashavu

Vanessa “Vee Money” Mdee tayari amerejea nyumbani Tanzania akitokea jijini Lagos, Nigeria alikoenda kutumbuiza kwenye tamasha la ‘Gidi Culture Festival’ lililofanyika Jumamosi iliyopita.

Vee Naija
Vanessa akitumbuiza kwenye tamasha la Gidi Culture Lagos, Nigeria wiki iliyopita

Vee Money akiwa msanii pekee wa Tanzania aliyetumbuiza jukwaa moja na wasanii wakubwa wa Afrika akiwemo Awilo Longomba, M.I, Waje na wengine, ameelezea uzoefu alioupata awamu hii ikiwa ni mara yake ya pili kutumbuiza Nigeria.

“Kusema kweli tumepokelewa vizuri sana ni tofauti na vile nilivyoenda mara ya kwanza, this time nimepata nafasi ya kufanya promo na media nyingi kwa wingi sana, na kwasababu wimbo wangu wa ‘Nobody But Me’ ndio kwanza umetoka kidogo watu wamekuwa wametazama kwenye mitandao na kwenye TV na wanaijua so ilikuwa tofauti na pale mwanzoni so ni hatua nyingine kwenye muziki wangu na muziki wa kizazi kipya wa kitanzania.” Vee Money aliiambia Millardayo.com.

Vanessa amesema kuwa alitumbuiza mbele ya mashabiki wa Nigeria wapatao 20,000 kwenye tamasha hilo lililofanyika ufukweni.

“Crowd ilikuwa kubwa style ya Fiesta yaani watu wengi sana kwanza show ilikuwa mchana na usiku, wapo wasanii walioperform mchana wengine waliperform usiku sisi ndio tulikuwa wa usiku lakini mchana walikuwepo kama watu elfu saba elfu nane, halafu usiku wakazidi wakawa kama kama elfu ishirini.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents