Technology

Video: Ifahamu Chizika, App ya kusikiliza muziki kwa simu iliyotengenezwa na watanzania

Ulimwengu wa sasa wa muziki umehamia kwenye smartphones. Kwa Ulaya na Marekani wapenzi wa muziki kwa sasa wanasikiliza zaidi nyimbo wazipendazo kwenye platform maarufu kama vile Spotify, Apple Music, Tidal na zingine.

11356960_388937114632648_737681832_n

Mtumiaji wa app hizo hufanya malipo kwa mwezi au mwaka na kuwa na uwezo wa kusikiliza mamilioni ya nyimbo. Tanzania nayo haiku nyuma.

Vijana wawili, Ali Makongo aka Young Siza na mtangazaji wa kipindi cha Daladala Beat cha Magic FM, Jimmy Jamal aka Jimmy Jay wameanzisha app ya muziki iitwayo Chizika ambayo kwa sasa inapatikana kwenye simu zinazotumia mfumo wa android.

App hiyo inamwezesha mtumiaji kusikiliza nyimbo pamoja na kutazama video za muziki za wasanii wa Tanzania.

“Lengo kubwa kabisa la kuanzisha Chizika App lilikuwa ni kuangalia jinsi gani wasanii wanaweza wakaingia kipato kutokana na muziki wao,” anasema Jimmy.

Wamesema Chizika App inamwezesha mtumiaji wa mtandao wowote kuitumia tofauti na app zilizoanzishwa hivi karibuni ambazo huwalenga wateja wa mitandao husika tu.

Mtumiaji anaweza kusikiliza muziki na kutazama video bure kwa dakika moja na kulipia kiasi kidogo cha fedha akitaka kusikiliza wote.

Malipo yanafanywa kwa njia ya simu.

Developer wa Chizika App, Ali Makongo amesema lengo lao ni kuifanya itumike na wapenzi wa muziki Afrika nzima.

App inapatikana Google Playstore. Tazama zaidi interview hiyo hapo juu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents