BurudaniVideos

Video: Lulu aeleza kwanini alilia siku anapokea tuzo ya AMVCA 2016

Elizabeth ‘Lulu ‘ Michael mwaka huu alishinda tuzo ya Best Movie East African kupitia filamu yake ‘Mapenzi ya Mungu’ kwenye tuzo za AMVCA 2016.

Wakati akishukuru kwa ushindi huo, muigizaji huyo alishindwa kuzuia kilio cha furaha kilichomkaba.

“Nadhani kilikuwa ni kitu ambacho kilitoka moyoni, hakikuwa kitu ambacho nilikitengeneza au nilipanga nikipata tuzo niongee hivi, I was also surprised and mimi niko emotional sana, so nadhani ni kitu kilichokuwa kinachotoka tu chenyewe moyo na ndio maana ilikuwa ni rahisi kumgusa mtu mwingine kwasababu it wasn’t fake, it was real,” ameiambia Bongo5.

Hata hivyo anasema kabla ya kushinda aliahidi kuwa angejikaza asilie lakini alishindwa kujizuia. Anadai usiku baada ya tuzo hiyo alikuwa na furaha iliyopitiliza kiasi ambacho alishindwa hata kwenda kwenye after party ya washindi wote.

Anasema ushindi huo umemfanya agundue jinsi kipaji chake kinavyothaminiwa na kwamba inambidi agundue kuwa ana kitu kikubwa.

Ijumaa Lulu ameachia filamu yake mpya iitwayo Ni Noma. Mtazame hapo chini akiizungumzia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents