BurudaniVideos

Video: Msanii wa Nigeria YCEE asema muziki wa Tanzania una nguvu Afrika

Hitmaker wa Omo Alhaji, YCEE kutoka Nigeria, amedai kuwa muziki wa Tanzania miaka ya hivi karibuni umekuwa na nguvu Afrika.

YCEE_TINNY-6

Akiongea na waandishi wa habari Jumatatu hii jijini Dar es Salaam, YCEE ambaye jina lake halisi ni Oludemilade Martin Alejo amesema kuwa hiyo ni sababu kubwa iliyomfanya aje Tanzania.

“Muziki wa Tanzania miaka ya hivi karibuni umekuwa ukipenya kwenye bara la Afrika sababu ya wasanii kama Diamond, Alikiba, wasanii wengine wanaendelea kujulikana kimataifa. Hivyo ukaaji wangu hapa ni kwaajili ya kufanya interview na vituo maarufu vya redio na TV. Nimesikia pia kuwa nina mashabiki hapa na muziki wangu unachezwa, hiyo ni sababu ndio maana kwanini tuko hapa kuanganika na watu na pia wasanii.”

“Kwa upande wa Diamond na Alikiba, muziki wao ni mkubwa sana Afrika hivyo itakuwa ni hatua kubwa kwangu kufanya nao kazi na msanii yeyete wa Tanzania anayefanya vizuri.”

Katika hatua nyingine, YCEE ametoa msaada wa shilingi milioni moja kwa kituo cha Kigamboni Community Centre. Atakuwepo Dar kwa siku tatu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents