Burudani

Video: Navio azungumzia album yake mpya ‘Power’ anayotarajia kuitoa mwezi huu

Daniel Lubwama Kigozi, maarufu kama Navio ni rapper kutoka Uganda ambaye amekuwa akifanya muziki kwa kipindi kirefu sasa toka alipoanzisha kundi lake la Hip Hop, Klear Kut na baadae kuanza kufanya muziki kama solo baada ya kundi hilo kujipa mapumziko ili rappers hao wamalizie masomo yao.

Navio

Rapper huyo hivi karibuni alikuwa nchini Nigeria akiendelea kujitangaza pamoja na kupromote album yake mpya inayokuja.

Kupitia ‘My Music & I’ ya Soundcity TV, Navio amezungumzia album yake mpya ‘Power’ anayotarajia kuitoa mwezi huu (Novemba) kupitia label yake ya Navcorp.

Amezitaja baadhi ya nyimbo ambazo zitapatikana kwenye album hiyo ikiwemo collabo yake na mwimbaji wa Nigeria Burna Boy inayoitwa ‘Besile’ ambayo walirekodi Uganda.

Wimbo mwingine utakaokuwemo kwenye album hiyo ni collabo yake na Mr Blue ‘Ayaya’ ambayo tayari imetoka pamoja na video yake.

Wimbo mwingine unaitwa ‘Cold Rider’ ambayo video yake imefanyika Miami, Marekani.

Wengine aliowashirikisha ni rapper wa kike wa Uganda, Keko pamoja na Ricardo Banks wa Ghana..

Mtazame hapa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents