Burudani

Video:Mpoto asema albam ya Waite imeingiza milioni 10, azungumzia kuhudhuria tuzo za ‘Afrima’ Marekani

Msanii wa muziki wa asili nchi,Mrisho Mpoto ambae ametajwa na Afrima nchini Marekani kuwania tuzo katika kipengele cha Best Traditional Artist, amefunguka kwa kusema kuwa mpaka sasa ameuza albam ya ‘Waite’ zaidi ya kopi eflu nane zenye thamani ya zaidi shilling milioni 10.
1521747_272787059512591_2006624544_n

Akizungumza na bongo5 leo, Mpoto amesema kilichomsaidi kwenye mauzo ya ablam ni tour ambazo alikuwa anafanya katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.

“Unajua kunatoafauti ya mashabiki na watu ambao ni wafuasi wako, watu ambao wanaku-support , mimi watu wanao ni-support, nikiangalia background yangu, nikiangalia mails ambazo napata , nikiangalia kwenye facebook yangu watu ambao wana like ,wana comment, wale ni watu wangu ambao ni wengi sana , kwaiyo nikasema hawa watu nikiwahesabu ninaweza nikawauzia albam yangu, kwaiyo mimi nakuwaga sina wasi wasi na soko , kwa sababu mimi soko langu ni la rika zote, watoto, vijana, wazee, wasomi na hata ambao hawajapata bahati ya kwenda shule, nimekuwa nikitembea kwenye tour zangu na nimeshauza copy nyingi sana, mpaka tulipo maliza Sabasaba nimeuza copy elfu nane, kwa sababu elfu tano nilikuwa nimeuza katika vyuo mbalimbali, na copy kama elfu mbili na kitu nimeuza kwenye kipindi cha Sabasaba, nimepata siyo chini ya milioni kumi(10)” Alisema Mpoto.

Wakati huo huo Mpoto amezungumzia mwakilo wake wa kwenda kwenye utaoaji wa tuzo za Afrima nchini Marekani ambazo ametajwa kuwania kipengele cha Best Traditional Artist.

“Nilipokea simu ilikuwa inatokea huko Marekani , walikuwa waniuliza kama mimi ndo Mrisho Mpoto, nikawaambia ndo mimi, wakaniambia kwamba unafahamu chochote kuhusiana na Afrima , nikawaambia nafahamu, ni tuzo ninazofanyika huko Marekani, akasema sawa hapa unaongea na director wa hizo tuzo na wewe umechaguliwa katika kipengele cha Best Traditional Artist, kwanza tunakupongeza na tutakuandikia emil, kukutumia certificate kwa sababu kwetu wewe ni mshindi, lakini pili tutakupa utaratibu wote wa jinsi ya wewe kusafiri, hotel na jinsi itakavyokuwa, kwaiyo Watanzania naomba muendelee kunipigia kura, lolote linaweza kutokea, tembelea tovuti ya Afrima alafu unichague” Alimalizia Mrisho Mpoto.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents